MBINU KUU TATU ZA KUKUSAIDIA KUONGEZA UFANISI WA KAZI KATIKA BIASHARA YAKO.

0
78

 

Waeza kua unajiuliza ni mambo gani ufanye kuwavutia wafanyakazi wazuri kwa ajili ya biashara yako? Utakiwi kubahatisha tena.Acha tukufahamishe.

 

Kati ya changamoto kubwa bosi yeyote ukumbana nayo, ni changamoto inayoitafuna na kuisumbua kampuni au biashara kwa mda mrefu ni kuwa na uwezo wa kuvutia na kuwatunza wafanyakazi bora na wenye uwezo.Mtandao wa ajira wa Linkedin umeripoti kua mwaka 2017 asilimia 10.9 ya watumiaji wake walibadilisha kazi ama ajira zao. Je hii ina maana gani kwa biashara ama kampuni yako?

Kawaida kutokana na mabadiliko ya kiteknolojia dunia na upungufu wa ajira nyingi kutokana na ongezeko la matumizi ya kompyuta duniani,Inasemekana ongezeko la upungufu wa wataalamu litaongezeka hii ikiwa hasa katika sekta za afya na sekta ya masuala ya fedha.

Hivyo hii imepelekea utafiti kufanyika na kugundua njiaa kuu makampuni makubwa yanazotumia kuvutia na kuwatunza wafanyakazi wenye vipaji ili kukuza uzalishaji.kwani mabosi hawa hujikita katika kuwapatia mahitaji yote muhimu wafanyakazi wao ili wafanyakazi wao waweze kujitoa na kuwajibika katika shughuli za kampuni.

MBINU HIZO NI HIZI;

1.WAPATIE WAFANYAKAZI WAKO WANACHOHITAJI

Hii inakuhitaji kwanza kujua haswa vitu wanavyoviitaji.Njia pekee ya kujua mtu anachohitaji ni kupitia kuzungumza nae, hivyo jitahidi kuwa na mazungumzo ya mara kwa mara na wafanyakazi wako kupata jua mahitaji yao haswa muhimu na kuyatenedea kazi kwa manufaa yao.

Hivyo ni vitu gani watu unaofaanya nao kazi wanahitaji ili waweze kufanya kazi kwa ufanisi zaidi, ni rahisi sana kama kuboresha aina ya chakula wapatacho mchana wawapo kazini, kuwaanzishia miradi ya kuwaendelezea kiutalaamu zaidi kupitia kuwaingiza katika programu kadha w kadhaa, kuboresha huduma ya upatikanaji wa maji ya kunya wakati wa kazi, kutafuta kujua nani anapitia wakati mgumu unaohitaji kusikilizwa na kujaliwa zaidi mfano kufiwa, kuuguliwa na mtu wa karibu, kuumwa, ama kujifungua na hivyo kuwatengenezea mazingira ya kazi katika namna wanayohisi kampuni imewajali sana hivyo yote hii hupelekea watu kuvutika kufanya kazi kwa ufanisi zaidi na kujali sana.

2.FIDIA MUDA WAO KWA NAMNA INAYOGUSA ZAIDI

Kipindi ambacho kazi kaika kampuni ama biashara zinaongezeka hivyo wafanyakazi kufanya kazi nyingi hata kuhisi kuanza choshwa na hali ya kikazi ofisini, ni muda ambao mabosi hutumia kuwafidia wafanyakazi wake kwa zawadi kama fedha, safari za kikazi mahali tulivu, chakula cha pamoja hoteli flani, kuwabadilishia mlo wa mchana kwa mda flani hivi kama namna ya kuwafanya wajihisi kujaliwa sana kiasi kuongeza ufanisi katika kazi.

3.WAPE UHAKIKA WA KESHO YAO

Wafanyakazi ni binadamu na kama wandamu wana hulka yakuwa na uhakika na kesho yao,hivyo ni jukumiu la bosi kuwa wa kwanza kuwaonesha mipango mikakati ya niashra ama kampuni ndani ya miaka kadhaa ijayo na haswa waapi kampuni inatakiwa ifike ndani mda flani hivyo hii kuleta uhakika wa kesho yao katika hayo wafanyayo, uhakika wa kesho uja pale wanapoona kupanda kwa vyeo na mishahara kwa wafanyakazi wa mda mrefu ndani ya kamuni. Hivyo uhakika wa kesho unapopatikana ufanisi huongezeka kwani hawana hofu ya kupoteza chochote na tayari wa kujitoa zaidi kwa ajili ya kazi unakuepo na hii kukuza uzalishaji

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here