“Wakati tunaanza biashara ,bidhaa nyingi za vyakula tulizokuwa tunaziona zilikuwa zinatoka nje ya nchi” Hayo ni maneno ya Jennifer Bash Maarufu kama Mama Alaska Tanzania,Mwanamke mjasiriamali katika sekta ya kilimo na Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya AKTZ maarufu kama ALASKA TANZANIA .

Jennifer Bash (mama Alaska) ambaye ni mhitimu wa shahada ya Masoko ya Kimataifa kutoka chuo cha Baruch Jijini New York,nchini Marekani pamoja na Elimu ya juu ya ujasiriamali na Usimamizi wa Biashara kutoka chuo cha Dar es salaam (UDSM) .Baba yake alikuwa mfanyabiashara kiasi kwamba Jennifer anahisi atakuwa amerithi Tabia na uwezo wa kibiashara kutoka kwa baba yake .hivyo historia ya maisha yake imekuwa mchango mkubwa na sahihi kabisa katika kumtengeneza yeye kuja kuwa mjasiriamali mwenye mafanikio na mwenye ushawishi na hamasa kw a vijana wengi haswa wakike nchini Tanzania.

Kampuni ya Alaska Tanzania ilianzishwa mwaka 2011 mwezi march na kuanza rasmi Utendaji wake Mwaka 2012 Mwezi November,ikianza na bidhaa ya mayai ya kwenye vifungashio yaliyouzwa katika supermarkets na miaka michache baadae wakafanikiwa kuongeza bidhaa nyingi zaidi kuanza Michele,mafuta,maharage,mayai,unga,na mazao mengine ya vyakula.Ambapo Alaska Tanzania ni Kampuni inayojihusisha na uzalishaji,upakiaji wa mazao ya chakula katika vifungashio vyenye kuongeza thamani ya mazao (packaging) pamoja na kusambaza mazao hayo,Na inafanya kazi na wakulima wadogo wadogo ambao kupitia Uwepo wa Alaska Tanzania wamejipatia solo LA uhakika LA bidhaa zao na hii inaipatia Alaska Tanzania bidhaa za kutosha kwa ajili ya kuzisambaza katika soko kubwa zaidi.

“Changamoto ndio fursa za mafanikio zikitumika vema” Msemo huu ni uthibitisho tosha wa alichokifanya Mama alaska kwani Anasema alipotoka masomoni Marekani alikuta bidhaa nyingi zinazopatikana kwenye supermarkets zilikuwa ni zile zinazotolewa nje ya nchi,na hii ilimfanya ajiulze kwani hatuwezi zalisha bidhaa zenye ubora toka ndani ya nchi ,vitu kama Michele,mayai,maharage mpaka tuagize nje ya nchi? ,na hivyo aliamua kufungua kampuni kutatua changamoto hiyo na kuwapa fursa na soko LA uhakika kwa wazalishaji wadogo wadogo wa bidhaa za kilimo,ambazo hivi sasa wanawauzia AKTZ  kwa ajili ya kuzifungasha katika vifungashio sahihi na kuziongezea thamani na ubora stahiki kwa ajili ya solo LA kimataifa na supermarket .Hivyo anawaasa vijana kuacha kulalamika na kuanza zigeuza changamoto kuwa fursa za mafanikio.Kwani vile vitu unavyoviona haviendi sawa vinaweza kuwa ndio wazo LA biashara kwako endapo utachukua hatua kutafuta namna ya kuviweka sawa na kutengeneza biashara katika changamoto hizo.

VITU VYA KUZINGATIA UNAPOANZISHA BIASHARA.

Yafuatayo ni baadhi ya mambo ambavyo anaamini mjasiriamli yeyote akiyazingatia na kuyatendea kazi ana uwezo wa kuanzisha biashara na kuikuza iwe kubwa sana kama yeye alivyofanya.

1.Hakikisha biashara yako inatatua tatizo Fulani katika jamii ama inarahisisha upatikanai wa huduma ama bidhaa Fulani katika jamii yako”.Kama ambavyo Alaska Tanzania Imejitahidi kurahisisha upatikanaji wa soko LA bidhaa za vyakula kwa wakulima wadogo wadogo na kutatua changamoto ya upatikanaji wa bidhaa za vyakula katika supermarkets vinavyotoka ndani ya nchini ,basi inawezekana hata kijana yeyote yule kuwa na biashara inayotatua changamoto katika jamii yake.

2.”wekeza katika kui-brand biashara yako na vifungashio vua bidhaa zao view vyenye ubora stahiki” Ni muhimu kuzingatia kuitengenezea sifa stahiki na muonekano Wenye kuaminika wa bidhaa zao na boashra yako kiujumla kwani wateja wanavutiwa na bidhaa ama biashara zilizo nadhifu katika mazingira yake na vifungashio vinavyotumika kufungia bidhaa hizo.

3.”Wekeza katika kujitangaza na kukuza soko LA bidhaa yako” Biashara yeyote haiwezi kukua isipokuwa soko lake linakua na kupanuka na njia rahisi na sahihi ya kukuza biashara yako ni kupitia kuitangaza na kuitengenezea sifa nzuri katika jamii ,ingawa zoezi hili huwa ni gharama sana lakini uwekezaji  katika kujitangaza kuja faida na manufaa makubwa katika kuongeza wateja na kupanua soko LA biashara husika.

4.”Muda ni pesa” Anashauri wajasirimali wadogo kuenda na muda na kutimia muda wa Leo kuwaza na kuweka mikakati kwa ajili ya kesho yao na ya biashara zao.

5. “Ubora wa huduma ama bidhaa ndio kivutio pekee cha wateja katika BIASHARA yeyote ile” Hakikisha unazalisha na kutoa huduma zenye ubora wa hali ya juu katika gharama anayoiumudu mteja wako,usitoe bidhaa ama huduma ili mradi Bali to a kitu kilicho bora kwani ndio kivutio cha mteja katika biashara yako.

Mwisho,Mama Alaska amekua mfano hai wa wanawake makini na viongozi wanaopenda kusaidia wengine kuwa watu bora zaidi na hii linathibitika kupitia programu  yake ya Mama Lishe inayotoa mafunzo ya kijasiriamali kwa wakina mama nchini Tanzania na pia kupitia harakati zake zingine amekuwa akitoa hamasa kwa vijana kuzidi kupambana ili ifike Siku wapate timiza ndoto zao kwani anaamini kila mmoja ana nafasi na uwezo wa kutendea kazi ndoto zake na kuzitimiza

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here